Akamatwa kwa kumuweka mama yake kwenye jokofu nyumbani kwa miaka 10

 


Polisi nchini Japan wamemkamata mwanamke mmoja baada ya mwili wa mama yake kukutwa kwenye jokofu nyumbani kwake.

 

Yumi Yoshino, 48, amesema kuwa alimkuta mama yake akiwa amefariki kisha aliuficha mwili wake miaka 10 iliyopita kwa sababu ” hakutaka kuhama” katika nyumba waliokuwa wakiishi mjini Tokyo, vyombo vya habari vimeripoti, vikinukuu maafisa polisi ambao hawakutajwa majina yao.


Hakukuonekana majeraha yoyote kwenye mwili ulioganda barafu, polisi wameeleza. Mamlaka hawakuweza kuthibitisha muda na sababu ya kifo cha mwanamke huyo. Mwili uliripotiwa kugundulika na mfanya usafi baada ya Bi. Yoshino kulazimishwa kuondoka katika nyumba hiyo kwa sababu ya kukosa kodi.


Mwili ulikuwa umekunjwa kiasi cha kutosha kuingia kwenye jokofu lenye barafu, polisi walisema. Bi Yoshino alikamatwa katika hoteli mjini Chiba karibu na jiji la Tokyo, siku ya Ijumaa.



from UDAKU SPECIAL BLOG https://ift.tt/2M8toX9
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI