Barbara: Kesi ya Yanga na Morrison Bado Ipo, Bado Wanahangaika Kama Wameachwa na Mpenzi




OFISA Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba, Barbara Gonzalez amethibitisha kuwepo kwa kesi kati ya Klabu ya Yanga na mchezaji wao, Bernard Morrison na kusema kuwa kwa sasa sakata hilo lipo mikononi mwa wanasheria wao ambao wanalishughulikia.


Tangu asajiliwe na Simba katika usajili ulioonekana kuwa na utata Morrison amekuwa akikumbana na vipingamizi vingi kutoka kwa waajiri wake wa zamani Yanga, huku kesi iliyopo CAS ikitajwa kuwa sababu kubwa ya kushindwa kuonekana kwa mchezaji huyo uwanjani kwenye michezo ya kimashindano tangu Desemba mwaka jana.



Hivi karibuni uongozi wa Yanga chini ya Makamu Mwenyekiti wa klabu hiyo, Fredrick Mwakalebela ulikiri kupeleka kesi hiyo kwenye mahakama ya kimataifa ya usuluhishi wa michezo CAS, ambapo Yanga wamesema shauri hilo linatarajiwa kusikilizwa hivi karibuni.


Akizungumzia kuhusu sakata la mchezaji huyo Barbara alisema: “Kesi ya Morrison na Yanga kweli bado ipo na wanasheria wetu wanashughulikia.“


Naona Yanga bado wanahangaika, ni kama upo kwenye mahusiano na mtu halafu mnaachana lakini wewe unalazimisha arudi wakati yeye hakutaki na ameshaendelea na maisha mengine.”



from UDAKU SPECIAL BLOG https://ift.tt/3cqJtCe
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI