DR Abbas: Ukitaka jifungie Serikali haitafungia watu ndani kisa corona


Dar es Salaam. Serikali imetoa msimamo wake kuhusu Covid - 19 kwamba, haitachukua uamuzi wa kuwafungia Watanzania ndani, huku ikitoa maelekezo ya kuendelea kuchukua tahadhari.


Hayo yamesemwa leo Jamapili Januari 31, 2021 na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dk Hassan Abbas wakati akizungumza na vyombo vya habari jijini Dodoma, kuelezea mambo mbalimbali yanayotekelezwa na Serikali ya awamu ya tano.


Amesema mwongozo wa Serikali kuhusu kile kinachoendelea duniani kuhusu Covid - 19 ni kuendelea kuchukua tahadhari kama ilivyotamkwa na Rais wa Tanzania, John Magufuli wakati wa ziara yake Kanda ya Ziwa wiki iliyopita.


“Kifupi cha ugonjwa wa virusi vya corona ni Covid - 19 ndiyo Kiswahili sanifu, Rais amesisitiza duniani ugonjwa unaendelea na kwa sababu ya maingiliano baina yetu na nchi zingine ni lazima tuendelee kuchukua tahadhari.


“Watanzania waendelee kuchukua tahadhari zote lakini tusiwe na woga wala tusichomekewe mawazo na mikakati ya watu wengine,” amesisitiza Dk Abbas.


Amesema ijapokuwa nchi inapambana kiuchumi kuna watu bado wana mawazo ya kufungiwa ndani.


“Tanzania haitafungiwa ndani shughuli ziendelee kama kawaida zile za burudani, michezo, ofisini mashambani ziendelee inapobidi kuchukua tahadhari maana kuna mtu yeye anatamani tu kwamba itangazwe amefungiwa ndani, wewe ukiona hutaki kutoka nje jifungiwe mwenyewe lakini msimamo wa Serikali haitafungia watu ndani,” amesema Dk Abbas ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari.



from UDAKU SPECIAL BLOG https://ift.tt/39B11tl
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI