Hofu ya bomu kwenye msikiti Uswidi

Kisanduku kinachofanana na bomu kimepatikana kwenye mlango wa msikiti mmoja uliopo katika mji mkuu wa Stockholm nchini Uswidi.

Imam wa Msikiti wa Stockholm, Mahmoud Khalfi, alitoa  maelezo kwenye kituo cha SR cha redio ya serikali nchini Uswidi na kusema kwamba walikuta kisanduku kinachofanana na bomu kilichowekwa kwenye mlango wa kuingilia msikitini na kuzua hali ya wasiwasi. Khalfi alisema,

“Tulipofika kwenye sala ya asubuhi, tuliona kisanduku kiinachofanana na bomu mlangoni. Nyaya zote 3 kutoka kwenye kisanduku hicho ziligandishwa mlangoni. Tuliwajulisha polisi haraka ambao baadaye walitenganisha kisanduku na nyaya zake na  kuchukua ili kufanyia uchunguzi.”

Akibainisha kwamba misikiti yake imekuwa ikishambuliwa mara kadhaa, Khalfi alisema kuwa wao wamekuwa walengwa wa mashambulizi ya kibaguzi zaidi ya mara mbili kwa mwaka.

Msemaji wa Polisi wa Stockholm Per Fahlström, aliarifu kugunduliwa kwa mtu aliyeweka vifaa hivyo kupitia kamera za usalama na kwamba uchunguzi unaendelezwa.



from UDAKU SPECIAL BLOG https://ift.tt/2LakKXC
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI