Kaze Akisuka Upya Kikosi Chake



KOCHA Mkuu wa Yanga Mrundi, Cedric Kaze ameanza program ya kukinoa kikosi chake kwa kuwatengeneza kisaikolojia nyota wake Said Ntibazonkiza ‘Saido’ na Tuisila Kisinda baada ya kutoka katika mapumziko kwa lengo la kuendelea na kasi waliyoanza nayo mwanzoni mwa msimu.Yanga ilianza vema msimu huu kwa kucheza michezo 18 bila ya kupoteza ikishinda 13 na sare tano pekee.

Yanga inayoongoza kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 44, juzi iliingia kambini huko kijiji cha Avic Town, Kigamboni jijini Dar es Salaam tayari kwa kuendelea na michezo ya ligi wakiwa wameliimarisha benchi lao la ufundi.

Akizungumza naChampioni Jumamosi,mara baada ya kuanza mazoezi alifanya kikao na wachezaji wake na kikubwa kusahau likizo fupi ya siku kumi aliyowapa mara baada ya kutoka kwenye Kombe la Mapinduzi na badala yake wafahamu wamerejea katika majukumu yao ya kazi.Kaze alisema mara baada ya kikao hicho taratibu aliona mabadiliko makubwa ya wachezaji wake kwa kurejea katika hali yao ya kawaida katika mazoezi yake ya Jumatano na Alhamisi.

Aliongeza kuwa ana matumaini makubwa ya nyota wake kurejea katika ubora wao ndani ya siku saba kuanzia juzi Jumatano baada ya kuona mabadiliko.

“Kwa hivi sasa kazi kubwa ninayoifanya ni kuirejesha saikolojia ya wachezaji wangu katika hali yao ya kawaida baada ya kutoka katika mapumziko mafupi ya siku kumi.“Hivyo wachezaji wangu hivi sasa wanachotakiwa kukifanya ni kusahau ambayo amewapata na kuanza majukumu mapya kwa kasi na zaidi ni kurejesha utimamu wa miili yao kabla ya kuanza ligi.“

Ninaona kwamba wachezaji wanazidi kurejea kwenye ubora ila haitakuwa kwa haraka lazima waanze taratibu kabla ya kurejea kwenye ule ubora ambao wamekuwa nao awali,” alisema Kaze.

Aidha mtu mmoja kutona ndani ya benchi la ufundi Yanga, aliliambia Championi Jumamosi kuwa, kwa sasa wachezaji wamekuwa wakipambana baada ya kuibuka kwa ushindani wa namba hasa eneo la beki ya kati na ushambuliaji.

Kumbuka kwenye dirisha dogo, Yanga iliongeza wachezaji wawili ambao ni beki Dickson Job na mshambuliaji Fiston Abdoulrazack raia wa Burundi.

“Kwa sasa hali ya mazoezi ndani ya kikosi cha Yanga imebadilika kila mchezaji anaongeza juhudi ili kutetea nafasi yake, vita ya namba kwa sasa imeongezeka kutokana na kikosi kuwa kipana baada ya wachezaji wawili kuongezeka kila mchezaji amekuwa akihofia namba yake kwa kuwa kikosi kimekuwa kipana.“

Mwalimu amewataka wachezaji wote kuongeza juhudi uwanjani pia amefurahishwa na uwezo wa wachezaji katika mazoezi ambapo atakayeonyesha kiwango zaidi ndiye atakayepata nafasi, kila mmoja ameonekana kuwa makini kujituma mazoezini ili wasipoteze nafai,” alisema mtoa taarifa.

Kikosi cha Yanga kiliingia kambini sambamba na kuanza mazoezi Jumatatu ya wiki hii ikiwa ni kwa ajili ya maandalizi ya michezo ya ligi iliyopangwa kuanza Februari 13, mwaka huu na Kombe la FA ambalo wamefuzu hatua ya 32 bora.

Stori: Wilbert Molandi na Khadija Mngwai, Championi



from UDAKU SPECIAL BLOG https://ift.tt/3r6NWhh
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI