Kumbe BongoFleva inalipa!! Diamond Platnumz anaingiza Milioni 200 kwa mwezi kwa matangazo tu

 


Msanii wa Bongofleva, Naseeb Abdul maarufu Diamond Platnumz amesema kila mwezi huingiza Sh200 milioni kutokana na kuingia mikataba na kampuni mbalimbali kuwa balozi wa bidhaa zao.


Akizungumza katika kipindi cha TheSwitch kinachorushwa na redio ya Wasafi leo Alhamisi Januari 28, 2021, Diamond amesema fedha hizo ni mbali na zile anazoingiza kupitia muziki.


Amebainisha kuwa anaingia mikataba na kampuni na amekuwa akifanya hivyo kwa kila kampuni inayohitaji huduma yake.


“Endosment zangu mimi mshahara wangu kwa mwezi si chini ya milioni 200, na tunasaini mikataba kila siku. Ninaingiza kwa wiki Sh55 milioni kwa siku Sh7 milioni kwa saa moja Sh300,000 na kwa sekunde Sh6,000.”


Amesema mwaka 2021 fedha anazozipata katika eneo hilo huenda zikaongezeka kwa kuwa anatarajia kuwa balozi wa vitu vingi zaidi kwa kuwa ameamua kufanya muziki kuwa kazi na biashara.



from UDAKU SPECIAL BLOG https://ift.tt/36wdT1X
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI