T.I Ajibu Tuhuma za Kuwadhalilisha Wanawake Kingono 'Mimi na Mke Wangu Hatujawahi Husika na Biashara ya Ngono Wala Kubaka"


 T.I. na mkewe wamevunja ukimya, wameibuka na kukanusha tuhuma za unyanyasaji wa kingono zilizotolewa na wanawake zaidi ya 25 wiki hii.


Rapa huyo ametumia njia ya video kuzungumzia suala hilo, amesema tuhuma hizo ni uongo na hazina ukweli wowote. "Kwa nguvu zote na hekima tunakanusha tuhuma hizi za kipuuzi zilizotolewa na watu wasiofahamika." ilisomeka caption kwenye video hiyo yenye dakika 8.


T.I. aliendelea kusema kwamba ilikuwa ngumu kuweza kukaa kimya kufuatia tuhuma hizi ambazo pia zinamchafua na mkewe Tiny Harris. Anaamini amechafuliwa (defamed) kwa sababu wanaomtuhumu hawajafungua shauri lolote mahakamani.

-

"Hatujawahi kumlazimisha mtu yeyote, hatujawahi kumuhusisha mtu yeyote kwenye masuala ya kingono, hatujawahi kumteka mtu yeyote pasina ridhaa yake. Hatujawahi kusafirisha chochote, yani kinachohusu biashara ya ngono." alisema T.I. na kukanusha pia tuhuma za kubaka, "Sijawahi kumbaka mtu yeyote, kamwe sijawahi kumbaka yeyote."



from UDAKU SPECIAL BLOG https://ift.tt/3j1sNT5
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI