Unaambiwa Serikali imeokoa Shilingi Milioni 389, Dr Gwajima Afunguka

 


Wizara ya Afya imeokoa takribani shilingi milioni 389 katika ujenzi wa jengo la Idara ya huduma za wagonjwa wa dharura linalojengwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora- Kitete ambalo limewekwa jiwe la msingi na Rais Dkt. John Magufuli.

Hayo yameelezwa jana na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzaia Dkt. John Pombe Magufuli, Dkt. Gwajima amesema ujenzi wa jengo hilo litakalo wahudumia wakazi wa Tabora, mikoa ya jirani na hata nje ya nchi kutokana na barabara kuu zinazopita mkoani hapo kwakuwa jengo hilo litakua na uwezo  kuwahudumia wagonjwa 50 hadi 60 tofauti na awali ambapo walikua wakihudumia wagonjwa 3 hadi 5.

"Tumepokea maelekezo yote yaliyotolewa na Mhe. Rais mimi pamoja na wizara yangu tutayafanyia kazi ikiwemo kuongeza madaktari bingwa, kuwafuatilia wale walioondoka pamoja na jengo la huduma la mama na mtoto kwa ajili ya kujifungua na ICU", amesema Dkt. Gwajima.


Miradi mingine ya ujenzi wa Idara ya huduma za wagonjwa wa dharura nchini ambayo wizara inashirikiana na Global Fund inatekelezwa na ipo hatua mbalimbali za kukamilishwa katika mikoa ya Ruvuma, Rukwa, Songwe, Mbeya, Iringa, Kilimanjaro, Njombe, Mara na Tanga.



from UDAKU SPECIAL BLOG https://ift.tt/2L4HQyF
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI