Baba Mzazi wa Young Killer afunguka mazito

 


EATV & EA Radio Digital imepiga stori na baba mzazi wa msanii wa HipHop Young Killer, anayefahamika kwa jina la Mzee Msodoki ambaye amesema chanzo cha kutokuwa sawa na mwanaye huyo ni mama yake kumwambia kwamba baba yake amefariki tangu utotoni.

 


Mzee Msodoki amesema mama Young Killer aliamua kumwambia hivyo mtoto wao kwa sababu aliumizwa na kitendo cha Mzee Msodoki kuukimbia ujauzito wa msanii huyo kabla hajazaliwa na kwenda kuishi nchini Congo DR.


"Mama Young Killer nilikuwa nakaa naye jirani kule Mwanza, wakati huo nilikuwa nafanya kazi Saloon, tukawa kwenye mahusiano ambayo yalidumu kama miezi 6 na baadaye akaniambia nina ujauzito, sasa kwa wakati huo mimi nilikuwa sijajiandaa kulea na majukumu hivyo nikapata safari ya kwenda Congo nilivyorudi sikumkuta" ameeleza Mzee Msodoki 


"Nimekuja kugundua kama mtoto yupo na ameshakuwa mkubwa ila mama yake alishamwambia kwamba baba yake ameshakufa wakati mimi nipo, ndiyo maana hata yeye haamini kama mimi ndiyo baba yake kweli" ameongeza 


Mzee Msodoki amesema aliwahi kukutana na Young Killer na alimwambia kama yeye ndiyo baba yake lakini alijibiwa kwamba hana shida lakini mpaka mama yake amdhibitishie



from UDAKU SPECIAL BLOG https://ift.tt/3kuiHKZ
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI