Hasira za Carlinhos Zamvuruga Kaze Yanga

 


UPO uwezekano mkubwa wa Kocha Mkuu wa Yanga Mrundi Cedric Kaze kukifumua kikosi chake cha kwanza na kumuingiza kiungo mshambuliaji Carlos Fernandez ‘Carlinhos’.


Kiungo huyo katika mchezo uliopita wa Ligi Kuu Bara ndiye aliyewafungia bao la ushindi dhidi ya Mtibwa Sugar akitokea benchi katika ushindi wa bao 1-0 walioupata kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar, lakini alionekana kuwa ni mwenye hasira na hakutaka kushangilia bao hilo.


Awali kiungo huyo alikuwa hapati nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo, licha ya kupona majeraha yake aliyokuwa akiyauguza na inadaiwa kuwa nicho ni chanzo cha kuwa na hasira ya kutopangwa wakati alikuwa fiti, ndiyo maana hata bao lake hakulishangilia.


Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Ijumaa, kutoka ndani ya kambi ya timu hiyo iliyoweka Avic Town, Kigamboni nje ya Dar kiungo huyo ameingizwa kwenye program na wachezaji wa kikosi cha kwanza katika mazoezi ya siku tatu wanayoendelea kuyafanya.


Mtoa taarifa huyo alisema upo uwezekano mkubwa wa Farid Mussa kuondolewa katika kikosi hicho cha kwanza na nafasi yake kuchukuliwa na Carlinhos katika kuelekea mchezo wao wa Kombe la FA utakaopigwa kesho Jumamosi Uwanja wa Mjapa, Dar.


Aliongeza kuwa kocha huyo amefurahishwa na utulivu, uwezo mkubwa wa kufunga mabao ndani na nje ya 18, hivyo vitu vimemvutia Mrundi huyo na kushawishika kumtumia katika michezo ijayo ukiwemo huo dhidi ya Kengold FC.“Katika safu ya ushambuliaji iliyokuwepo hivi ndani ya timu, Carlinhos ndiye ameonekana mtulivu akiwa ndani na nje ya 18 akiwa kwenye goli la wapinzani.


“Na hiyo ni baada ya bao lake la kiufundi alilolifunga na kutupa pointi tatu tulipocheza dhidi ya Mtibwa katika mchezo wa ligi tulioucheza juzi (Jumamosi iliyopita) kwenye Uwanja wa Mkapa.“


Hivyo, Carlinhos atakuwa sehemu ya kikosi katika mchezo ujao ambao timu inahitaji kupata ushindi na atamtumia kutokea pembeni akichukua nafasi ya Farid,” alisema mtoa taarifa huyo.


Kaze hivi karibuni alisema kuwa: “Anaamini uwezo mkubwa aliokuwa nao Carlinhos, lakini majeraha ndiyo yamemsababishia nimuondoe kikosini, ni mzuri zaidi akitokea pembeni na siyo katikati namba 10.”



from UDAKU SPECIAL BLOG https://ift.tt/3aTp1bY
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI