Jela miaka 30 kwa kumlawiti mtoto wa miaka 15

 


Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Serengeti imemhukumu Mageta Masaro (29) mkazi wa Nyakitono kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la kumlawiti mtoto wa miaka 15.



Hakimu mkazi mfawidhi wa Wilaya Serengeti,  Ismael Ngaile katika kesi ya jinai namba  117/2020 leo Ijumaa Februari 26, 2021 amesema ushahidi wa watu sita uliowasilishwa na Serikali haukuacha shaka.




Amesema kutokana na kukithiri kwa matukio ya ubakaji mahakama inalazimika kutoa adhabu kali ili iwe fundisho kwa watu wengine.




Mwendesha mashtaka wa Serikali, Renatus Zakeo amesema Aprili 24, 2020 mshtakiwa alimtumia binti aliyekuwa akiishi nyumbani kwao kumuita mtoto huyo mwanafunzi wa shule ya msingi Nyakitono na alipofika alimkamata na kumlawiti.




Amesema mtoto huyo alipiga kelele na wananchi wakajitokeza na kumkamata mshtakiwa, na mtoto huyo alipopimwa iligundulika kuwa amelawitiwa.




Alibainisha kuwa hawana rekodi ya matukio ya mshtakiwa lakini ameiomba mahakama itoe adhabu kulingana na kosa alilokuwa nalo.



from UDAKU SPECIAL BLOG https://ift.tt/2Ph1XeS
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI