Kauli ya Dkt. Bashiru baada ya kuapishwa Ikulu

 


Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Bashiru Ally, amemshukuru Rais Dkt. John Magufuli, kwa kundelea kumuamini huku akiwaomba Watanzania waendelee kumuombea ili aweze kukidhi matarajio ya Rais Dkt. Magufuli.

 

Kauli hiyo ameitoa hii leo Februari 27, 2021, mara baada ya kula kiapo cha kuwa Balozi na Katibu Mkuu Kiongozi, Ikulu Jijini Dar es Salaam, nafasi ambayo ilikuwa ikishikiliwa na Balozi John Kijazi, aliyetangulia mbele za haki Februari 17 mwaka huu.


"Leo siwezi kusema mengi kwa sababu mbili, ya kwanza ni kwa mazingira ambayo nimepata uteuzi huu, ulinipa kazi ambazo zingeweza kuchukua mwezi mzima na niongeondoka kesho au keshokutwa jana jioni napata taarifa kwenye mitandao kwamba umeniteua," amesema Balozi Dkt. Bashiru Ally


Aidha, ameongeza kuwa "Bado natafakari sana nitafanya nini na vipi ili kukidhi matarajio yako kwa imani uliyonipa kwa mfulululizo, niwaombe Watanzania wote mniombee ili niweze kukidhi matarajio ya Mh. Rais".


Kabla ya uteuzi huo hiyo, Dkt. Bashiru Ally, alikuwa ni Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM).



from UDAKU SPECIAL BLOG https://ift.tt/2NJgorE
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI