Kimenuka, Sibomana Naye Aipeleka Yanga Fifa





MSHAMBULIAJI wa zamani wa Yanga, Patrick Sibomana ameibuka na kudai yupo kwenye mpango wa kuifungulia mashitaka Klabu ya Yanga kwenye Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), kwa kile alichokieleza kuwa, ukiukwaji wa makubaliano ya malipo ya stahiki zake.

 

Hii inakuja ikiwa ni siku chache baada ya Fifa kuitaka Yanga kumlipa aliyekuwa mshambuliaji wa timu hiyo, Amissi Tambwe.

 

Sibomana aliichezea Yanga kwa msimu mmoja uliopita kabla ya kuachwa mwishoni mwa msimu huo.Akizungumza na Championi Jumamosi, Sibomana alisema: “Tulikubaliana kwamba Yanga wanilipe fedha zangu za usajili ambazo zilibaki kiasi cha dola 10,000 (Sh mil 23).

 

“Kwa kuwa niliishi nao vizuri na nilijua timu ilikuwa haina fedha, tulipanga wanilipe kwanza fedha ya miezi mitatu pamoja na fedha ya usajili ambayo jumla yake ni dola 16,000 (Sh mil 36.9) ambayo nilikatwa kodi hadi kufikia dola 14,500 (Sh mil 33.4).



“Tukakubaliana kwamba wangenilipa Oktoba 30, mwaka jana ambapo walinipatia dola 3,000 (Sh mil 6.9) ikabaki dola 11,500 (Sh mil 26.5) ambapo niliwaambia wanipatie zote, lakini cha kushangaza walinitumia dola 1,500 (Sh mil 3.4) na mwezi Januari mwaka huu wakanipatia pesa iliyobaki, ambapo deni likabaki dola 4,000 (Sh mil 9.2.

 

“Sasa mimi nilikwazika kwa sababu walikuwa wakinilipa kwa muda wanaotaka na kwa kiwango wanachotaka, kila nikiwatafuta viongozi wamekuwa wakiniambia kwa nini nawaandikia barua mara kwa mara, wakati inawezekana nikarejea kwao siku moja.“

 

Mimi naona wananionea, kwa kutofuata makubaliano tuliyokuwa nayo na sijui kwa nini? Hivyo kwa sasa tayari nimewaandikia barua Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), na kama suala langu litakuwa halijapatiwa ufumbuzi hadi kufikia Machi 1, basi sitakuwa na njia nyingine zaidi ya kupeleka malalamiko yangu Fifa.“Kiukweli nisingependa kufika huko, lakini nadhani wao ndiyo wananisukuma kufanya hivyo,” alisema Sibomana.

 

Alipotafutwa Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Haji Mfikirwa azungumzie ishu hiyo alisema: “Taarifa kuhusiana na madai ya Sibomana tunazo hivyo tunashughulikia.

 

”Ulipotafutwa uongozi wa TFF kuthibitisha taarifa hiyo, Ofisa Habari wa TFF, Clifford Ndimbo alisema: “Kwa upande wangu siwezi kusema lolote kwa sasa mpaka pale nitakapopata nafasi ya kuwasiliana na kamati ya sheria kuhusiana na hilo.


from UDAKU SPECIAL BLOG https://ift.tt/3bZ0odl
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI