Kocha Simba Aiwekea Mtego Yanga




WAKATI mbio za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu Bara zikiwa bado mbili, Kocha Mkuu wa Simba, Didier Gomes, amesema licha ya kushiriki mashindano mengi tofauti, lakini hawajasahau michezo yao mitatu ya viporo kwenye ligi hiyo ambayo wanataka kushinda ili kuishusha Yanga kileleni.

 

Hivi sasa Simba inakamata nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara ikiwa imekusanya pointi 42 baada ya kucheza mechi 18, ikizidiwa pointi saba na vinara wa ligi hiyo, Yanga wenye pointi 49 zilizotokana na kucheza mechi 21 ambazo ni tatu zaidi ya Simba.



Kesho Jumatatu, Simba inatarajiwa kushuka uwanjani kuvaana na JKT Tanzania katika mchezo wa kiporo wa ligi kuu, utakaopigwa Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.

 

Endapo Simba ikifanikiwa kushinda mechi zate tatu za viporo, basi itaishusha Yanga kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo na kukaa mabingwa hao watetezi kwa tofauti ya pointi mbili.

 

Akizungumza na Spoti Xtra,Gomes alisema: “Hivi karibuni ratiba yetu imetubana kidogo kwani tumekuwa na michezo mingi ya michuano tofauti, lakini ni jambo zuri kuona tunapata matokeo mazuri kwenye michezo yote.



“Licha ya michuano mingi tuliyonayo, lakini nikuhakikishie bado tunakumbuka kuwa tuna michezo mitatu ya ligi ambayo lazima tushinde, kwani tunataka kushika usukani wa ligi katika kipindi hiki ambapo ligi inaelekea ukingoni ili kujihak-ikishia malengo yetu ya kutwaa ubingwa msimu huu.”




from UDAKU SPECIAL BLOG https://ift.tt/3uDAvIm
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI