Mbwa watumika kukagua wagonjwa wa Covid-19 Finland



Mbwa waliofunzwa nchini Finland wana uwezo wa kugundua wagonjwa walio na maambukizi ya virusi vya corona (Covid-19).


Mbwa hao waliopewa mafunzo maalum wamekuwa wakitumika katika viwanja vya ndege nchini humo tangu Septemba, kudhibiti abiria kwa sababu ya Covid-19.  Kulingana na matokeo ya awali, kiwango cha usahihi ni kati ya asilimia 95 na asilimia 100.


Baada ya ukaguzi wa Covid-19 ambao unafanyika ndani ya dakika moja, abiria huruhusiwa kuendelea na safari zao kwa kutegemea na matokeo.


Katika mchakato wa ukaguzi, abiria hufuta shingo zao kwa vitambaa vya kufyonza, kisha vitambaa hivyo huwekwa kwenye makopo ambapo baadaye mbwa huja kufanya ukaguzi kwa kunusa upande wa pili wa kuta za makopo hayo.


Ikiwa matokeo yanaonyesha kuwa na maambukizi, abiria hupelekwa kwenye kitengo cha huduma za afya katika uwanja wa ndege.


Wakati wataalam wanadai kuwa matokeo ya mbwa ni ya kuaminika zaidi kuliko vipimo vya PCR,  Dr. Anna Hielm-Björkman kutoka kitengo cha matibabu ya wanyama cha chuo kikuu cha Helsinki alisema kuwa katika hali nyingine ambapo vipimo vya PCR ni hasi, watu waliogunduliwa kuwa na maambukizi na mbwa huonyesha dalili za ugonjwa baada ya siku chache.


Hielm-Björkman aliongezea kusema kuwa virusi vya Covid-19 haviwezi kuambukizwa mbwa na kwa hivyo hakuna wasiwasi  wowote, na kwamba idadi ya mbwa waliofunzwa inapoongezeka, mchakato huu unaweza kutekelezwa katika milango ya nyumba za wauguzi, shule, chekechea na maeneo mengine ya wazi ya umma.


Mbali na Finland, mbinu hii pia inatumiwa nchini Chile na Falme za Kiarabu.


Katika bara la Ulaya, ikiwa majaribio ya mbwa waliofunzwa huko Ufaransa na Ujerumani yatatoa matokeo mazuri, basi wataanza kutumika katika viwanja vya ndege



from UDAKU SPECIAL BLOG https://ift.tt/3qZkqKM
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI