Mobeto Aungana na Sarah Kumkabili Kajala

 


MWANAMITINDO wa kimataifa na msanii wa Bongo Fleva, Hamisa Mobeto, anadaiwa kuungana na aliyekuwa mke wa msanii mwenzake, Rajab Abdul ‘Harmonize’, Sarah Michelotti, IJUMAA WIKIENDA limedokezwa.

Kwa mujibu wa watu wa karibu wa Mobeto, kwa sasa kuna muunganiko mzuri kati ya Mobeto na Sarah ambaye alimwagana na Harmonize mwishoni mwa mwaka jana, kabla ya jamaa huyo kuibuka kwa staa wa Bongo Movies, Kajala Masanja ambao kwa sasa ndiyo kapo inayotetemesha zaidi kwenye mitandao ya kijamii

Sasa, ubuyu wa moto unaeleza kwamba, baada ya Mobeto kutibuana na Kajala kiasi cha kumuweka ndani kwa sababu ya lile sakata la mwanaye Paula kurekodiwa video chafu akiwa na msanii Rayvanny kisha kusambaa mitandaoni, basi bifu limekuwa zito kiasi cha kuomba msaada wa hali na mali kutoka kwa Sarah ambaye naye ana bifu na Harmonize kwa kuwa hawakuachana vizuri.

Gazeti la IJUMAA WIKIENDA limefuatilia nyendo za Mobeto na Sarah na kung’amua kwamba, kwa sasa ni mashosti walioshibana.

Ukaribu wao unadhirishwa na jumbe mbalimbali za majuto anazoziposti Sarah kwenye ukurasa wake wa Instagram ambapo Mobeto amekuwa miongoni watu wa mwanzomwanzo kuzisoma na ‘kuzi-like’ akionesha kuguswa nazo.

Gazeti la IJUMAA WIKIENDA limemtafuta Mobeto ili kujua kama ana ukaribu na Sarah ambapo hakutoa ushirikiano.

STORI; KHADIJA BAKARI, DAR



from UDAKU SPECIAL BLOG https://ift.tt/2ZShFPw
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI