MTU mmoja ameuawa na Jogoo wake aliyekuwa amefungwa kisu mguuni kwa ajili ya mchezo uliopigwa marufuku wa kupambanisha jogoo Kusini mwa India.

 

 

Mmiliki wa jogoo alichomwa kisu usawa wa kati ya tumbo na nyonga wakati kuku huyo akijaribu kutoroka. Mwanaume huyo alipoteza maisha akiwa njiani kuelekea hospitali kwasababu ya kupoteza damu nyingi.

 

 

Polisi hivi sasa wanawatafuta watu wengine 15 waliohusika kwenye tukio hilo, ambalo lilifanyika kwenye kijiji cha Lothunur jimbo la Telangana wiki hii, Kuku huyo alishikiliwa katika kituo cha polisi kabla ya kupelekwa shambani.

 

 

Polisi wamesema mnyama huyo alikuwa akitayarishwa kwa ajili ya kushiriki mpambano alipojaribu kutoroka. Mmiliki alijaribu kumkamata lakini alichomwa na kisu hicho chenye urefu wa sentimita 7 kilichokuwa kimefungwa kwenye mguu wa kuku huyo wakati wa purukushani hizo.

 



Wale waliohusika katika tukio hilo wanakabiliwa na mashtaka ya mauaji ya kutokusudia, kujihusisha na mchezo haramu wa kamari na kuhodhi mchezo wa kupiganisha kuku, shirika la habari la Ufaransa limeripoti.

 

 

Afisa polisi katika eneo hilo B Jeevan amesema kuku huyo atapelekwa mahakamani kwa ajili ya ushahidi, kwa mujibu wa gazeti la The New Indian Express.

 

 

Mchezo wa kuwapambanisha jogoo ulipigwa marufuku India mwaka 1960, lakini mchezo huo bado ni maarufu vijijini kama Telangana wengi hasa katika matamasha ya jamii ya Hindu wa Sankranti.

 

 

Si mara ya kwanza kwa mmiliki wa kuku kuuawa na jogoo wake, Mwaka jana mwanaume mmoja huko Andhra Pradesh aliaga dunia baada ya kukatwa shingoni na kiwembe kilichokuwa kimefungwa kwenye mguu wa jogoo.

 

 

Kwa mujibu wa Shirika la habari la CNN, mmiliki alikuwa akimchukua jogoo wake tayari kwa mpambano wa jogoo wakati tukio hilo lilipotokea.




from UDAKU SPECIAL BLOG https://ift.tt/3bIEhri
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI