Nandy Afanyiwa Hujuma Nzito

 


PISI kali kunako muziki wa Bongo Fleva, Faustina Charles Mfinanga ‘Nandy’, anadaiwa kufanyiwa hujuma nzito, IJUMAA WIKIENDA lina kisanga kamili.

 

Hujuma hiyo imeelekezwa kwenye wimbo wake mpya alioutoa na nguli wa muziki barani Afrika, Le Grand Mopao Koffi Olomide unaokwenda kwa jina la Leo Leo.

 

Inasemekana wimbo huo alioutoa kwa mfumo wa audi (sauti) umeshindwa kufikisha wasikilizaji milioni moja ndani ya wiki moja kwenye Mtandao wa YouTube kutokana na kiki zilizoingizwa mitandaoni kwa makusudi na kuufanya wimbo huo usiwe gumzo.

 

Watu wa karibu wa Nandy wanasema kuwa, Nandy ameshagundua njama hizo kuwa zilipangwa na watu ili kumuharibia kwa sababu wimbo wake huo ungekamata zaidi ya sasa pamoja na kwamba bado unasikilizwa mno na kutingisha mitandaoni.

 

Inaelezwa kwamba, washindani wake walipoona kuna kila dalili wimbo huo ukafunika nyimbo zote zilizotoka wiki iliyopita ndiyo maana ikatafutwa mbinu ya kuweza kuuzima moto wake.

 

“Unajua Nandy mwenyewe anajua wazi kwamba kuna hujuma imefanywa ili kumuharibia wimbo wake huo usiweze kusikika.


“Siyo siri, jambo hilo limemnyima mno usingizi kwa sababu mambo kama hayo ndiyo yanarudisha muziki wetu nyuma.

 

“Nandy ameamua tu kunyamaza na vile unavyomjua siyo mtu wa kuongea badala yake ameishia tu kusema hana la kufanya kwa sababu ametumia pesa nyingi sana (zaidi ya milioni 70) kuandaa wimbo huo,” kinasema chanzo chetu cha kuaminika.

 

Chanzo hicho kinazidi kupenyeza ubuyu kwamba, kitendo hicho ni hujuma kubwa mno kwa Nandy, lakini imebidi akubali kwa sababu watu wengi kwenye mitandao walikuwa wakifuatilia ishu za akina Rayvanny na mtoto wa Kajala, Paula na siyo kusikiliza kwa wingi huo wimbo wake ambao hadi jana ulikuwa na wiki moja na umesikilizwa mara zaidi ya laki saba pale mjini YouTube na kushika namba saba kwenye trending.

 

“Ila mimi naona kabisa hawakufanya vizuri kwa sababu wamesahau kabisa Nandy amewekeza pesa nyingi kiasi gani. Unajua kumleta mwanamuziki mkuwa kama Koffi siyo kitu cha mchezomchezo, lakini ndiyo hivyo wamemuangusha mwenzao, inauma mno na wamemuumiza sana Nandy, hajisikii vizuri,” anasema mtu huyo wa karibu na Nandy.

 

Gazeti la IJUMAA WIKIENDA lilimtafuta Nandy ili kuzungumza naye kuhusu ishu hiyo, lakini simu yake iliita bila kupokelewa na hata alipotumiwa ujumbe kwa njia ya WhatsApp ulionesha amesoma,


STORI; IMELDA MTEMA, DAR



from UDAKU SPECIAL BLOG https://ift.tt/2O6qaDQ
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI