Wanaswa na vipande 13 vya meno ya tembo wakisaka wateja





Kikosi maalum ya kupambana na ujangili katika eneo la ikolojia ya Tarangire – Manyara, kimewakamata watu wawili katika  kijiji cha Moyaka wilaya ya Babati mkoani Manyara wakiuza vipande 13 vya meno ya tembo.


Mkuu wa kikosi cha kuzuiwa ujangili (KDU) Kanda ya Kaskazini, Peter Mbanjoko leo Februari 28 amethiitisha kukamatwa watuhumiwa hao, Benard Masalu na  Yembeson Masumbuko na kupongeza kazi nzuri ambayo imefanywa na askari wa hifadhi ya Taifa ya Tarangire, Burunge WMA na Chemchem ambao wamewekeza katika eneo hilo.



“Nimepata taarifa za tukio hili na tayari watuhumiwa hao wanashikiliwa na jeshi la polisi na taratibu za kuwafikisha Mahakamani zinaendelea,” amesema.



Mtendaji mkuu wa Taasisi Chemchem Assosiation, Walter Pallangayo amesema kukamatwa kwa watuhumiwa hao kulitokana na taarifa za siri ambazo walizipata na wakaandaa mtego uliofanikisha kukamatwa kwao.



Taasisi ya Chemchem ambayo imewekeza hoteli za kitalii na kufanya utalii wa picha katika eneo la Burunge WMA imekuwa na mfuko maalum wa kupambana na ujangili ambapo kwa mwaka Sh400 milioni zinatumika  kufanya operesheni katika eneo hilo la ikolojia ya  Tarangire – Manyara.


from UDAKU SPECIAL BLOG https://ift.tt/3bRTvtU
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI