Adakwa akisafirisha Kobe 400 kwenye mabegi Simiyu




Jeshi la polisi mkoani  Simiyu linamshikilia mtu mmoja (jina linahifadhiwa) miaka 35 Mkurya mkazi wa Wilaya ya Bunda mkoani Mara kwa kosa la kukutwa akisafirisha Kobe 438 kwenye mabegi bila ya vibali.




Akiongea na Waandishi wa Habari leo Machi 31, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Richard Abwao, amesema kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa Machi 21, 2020 saa 2:00 usiku.



Kamanda Abwao amesema jeshi hilo lilipata taarifa kutoka kwa raia wema, ambapo mtuhumiwa alikamatwa akiwa anasubilia usafiri katika kata ya Dutwa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi mkoani humo.



Ameeleza kuwa baada mtuhumiwa kukamatwa, alikutwa akiwa na mabegi matatu yote yakiwa yamebeba wanyama hao, ambao alieleza thamani yao ni sh. Milioni 71,161,866.





“Mpaka sasa tunamshikilia mtuhumiwa kwa ajili ya mahojiano zaidi, tunataka kujua aliwatoa wapi na alikuwa anawapeleka wapi, tunataka kujua na mtandao mzima maana tunajua hayuko peke yake,” amesema Abwao.



Aidha Kamanda Abwao amesema kuwa jeshi hilo limekabidhi wanyama hao kwa maafisa maliasili kwa ajili ya kuhifadhiwa, huku wakiendelea kumshikilia mtuhumiwa na upelelezi ukikamilika atafikishwa mahakamani.



Hata hivyo Kamanda huyo wa Polisi amewataka wananchi kujiepusha na umiliki wa nyara za serikali kinyume na sheria kwani kufanya hivyo ni kosa la jinai.




from UDAKU SPECIAL BLOG https://ift.tt/3dloKOP
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI