Corona, kikwazo kwa Chelsea ligi ya mabingwa ulaya

 


Michezo miliwi ya ligi ya mabingwa barani ulaya hatua ya robo fainali kati ya FC Porto ya Ureno na Chelsea ya England itachezwa nchini Hispania katika Dimba la Ramon Sanchez-Pizjuan ambao ni uwanja wa klabu ya Sevilla , shirikisho la soka barani ulaya UEFA limethibitisha.

 

Timu zote mbili zitapoteza faida ya kucheza uwanja wa nyumbani, hii ni kutokana na kanunu za kujikinga na Covid-19 zilizowekwa na nchi zote mbili, ambapo wageni wote wanaoingia England kutoka Ureno ni lazima wakae karantini kwa siku 10, wakati huohuo Ureno nao hawapokei wageni kutoka England, hivyo isingekuwa rahisi kwa timu hizi kucheza michezo hii katika mataifa yao.


Taarifa iliyotolewa na UEFA imesema Tunapenda kuthibitisha mchezo wa hatua ya robo fainali wa ligi ya mabaingwa wa mkondo wa kwanza na wa pili unaohusisha timu za FC Porto na Chelsea , michezo yote miwili itachezwa nchini Hispania katika dimba la Ramon Sanchez-Pizjuan ambapo mchezo wa mkondo wa kwanza utachezwa April 7 na wapili utachezwa Aprili 13.


Lakini pia kwenye taarifa ya shirikisho hilo la soka Ulaya likaishukuru klabu ya Sevilla na chama cha soka cha Hispania kwa kukubali kuwa wenyeji wa mchezo huo.


FC Porto walikata tiketi ya kucheza robo fainali kwa kuiondoa Juventus kwa faida ya bao la ugenini, baada ya matokeo ya jumla kumalizika kwa sare ya mabao 4-4. Wakati Chelsea wao waliiondoa Atletico Madrid kwa ushindi wa jumla wa mabao 3-0.



from UDAKU SPECIAL BLOG https://ift.tt/3sHsn8u
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI