“Hatuoni tabu kuomba radhi kama tulitofautiana huko nyuma…..” – Kheri James Mwenyekiti UVCCM

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana CCM Taifa (UVCCM) Kheri James amesema UVCCM haioni tabu kuomba radhi kwa yeyote iwapo kuna mambo waliyafanya huko nyuma ambayo yalichochea chuki na uhasama na kuteteresha umoja na mshikamano wa Watanzania.


“Yawezekana katika siasa zetu na hekaheka zetu tuliweza kutofautiana kimitazamo, yapo mambo ambayo huko nyuma yalipelekea umoja wetu ukaterereka, UVCCM hatuoni aibu kusema tunaomba radhi kwa hayo kama tuliyatenda na tupo tayari kurekebisha ili kutengeneza jukwaa safi kwa Rais wetu kuanza upya akiwa na Watu walioshikamana na kuwa wamoja ili Nchi yetu iweze kwenda mbele”

“Sisi kama Vijana wa Mapinduzi kote Nchini tunao wajibu wa kushirikiana na Vijana wenzetu kuilinda dhamira hii ya Rais wetu ya kuwaleta Watanzania pamoja, kujenga mshikamano wao, kuzika tofauti zetu, ya kufungua kurasa mpya utakaotoa dira ya usawa, haki na maendeleo ya ukweli kwa Watanzania wote”

“Sisi Umoja wa Vijana CCM kamwe hatutokuwa kikwazo cha dhamira hiyo, kama kuna jambo huko nyuma ambalo kwa maneno au matendo ambalo linaweza kutumika kama rejea ya kuzuia hiyo dhamira ya Rais wetu sisi tunasema tunaomba radhi na tuko tayari kushirikiana na Rais wetu ili kuhakikisha dhamira yake haikwamishwi na matendo wala maneno yetu” – Kheri James.



from UDAKU SPECIAL BLOG https://ift.tt/3dgxMwJ
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI