Kauli ya Dkt. Mpango Baada ya Kupendekezwa Kuwa Makamu wa Rais





Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amempendekeza Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Machi 30, 2021.

 

 

Baada ya jina lake kupendekezwa kuwa Makamu wa rais,Dkt Philip Mpango ametoa hotuba ya nguvu iliyoibua hisia za Wabunge. Huku akisema “Kazi zote Njema ni Kazi za MUNGU.”

 

 

“Namshukuru sana Rais Samia Suluhu Hassan kwa kulipendekeza jina langu kuwa Makamu wa Rais, ni heshima kubwa sana, sikuwahi kuota, nimepigwa na butwaa.

 

 

“Napenda kumshukuru Mungu kwa namna ya pekee kwa kutupatia uhai na kutuwezesha kukutana hapa kuendelea na shughuli za kikatiba, na kipekee nimshukuru Mama Samia kwa kupendekeza jina langu na kuridhiwa na Chama chetu CCM.

 

 

“Ni heshima kubwa sana, sikuwahi kuota, nimepigwa na butwaa. Mimi ninaamini kuwa kazi zote njema ni kazi za Mungu, na kwa hiyo kazi njema tunawajibika kuzifanya kwa akili zetu zote na nguvu zetu zote kwa maslahi ya Taifa letu.

 

 

“Alipofariki Dkt. John Pombe Magufuli nililia sana hadharani na hata nyumbani na baadaye yalikauka kwa kuwa tunajua Taifa lisonge mbele. Lazima tuzisimamie rasilimali za nchi kwa macho yetu. Mimi ni mtoto wa maskini, na najua kiatu cha umasikini kinavyouma.

 

 

“Namna pekee ya kumuenzi Hayati, Dkt. John Magufuli ni kuyaishi yale yote aliyokuwa akiyatenda,” – Philip Mpango akizungumza baada ya kuteuliwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

 


from UDAKU SPECIAL BLOG https://ift.tt/3u8R6Tw
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI