Mwambusi Aunda Vikosi Vitatu Yanga





UNAAMBIWA kocha wa muda wa Yanga, Juma Mwambusi, amedhamiria kufanya kweli kwenye michezo iliyosalia baada ya kukigawa kikosi hicho kwenye makundi matatu ili kutengeneza silaha ya kupata mabao.

 

Mwambusi amekuwa akiigawa Yanga makundi matatu kwenye mazoezi ya timu hiyo, ambapo kuna kundi kazi yake kukaba, kundi lingine kutengeneza nafasi za mabao na kupiga krosi huku kundi lingine likiwa na kazi ya kufunga tu.



Beki wa kati wa timu hiyo, Dickson Job, aliliambia Championi Jumatatu kuwa, Mwambusi amekuwa akitengeneza uwiano wa timu kwa kufanya mazoezi ya mbinu ya kukaba na kufunga, zoezi ambalo limekuwa likifanyiwa kazi vizuri na wachezaji.



“Kimsingi kambi yetu inakwenda vizuri sana, kwa sababu kocha amekuwa akisisitiza timu kwenye kukaba, kutengeneza nafasi za mabao na kufunga kila wakati nafasi inapopatikana jambo ambalo tumekuwa tukilifanyia kazi mara kwa mara na kutoa matokeo chanya,” alisema Job.

 

Yanga wanafanya mazoezi kwenye uwanja uliopo Avic Town Kigamboni, sehemu ambayo pia wameweka kambi yao kwa muda wote tangu kuanza kwa msimu huu.

STORI: ISSA LIPONDA, Dar es Salaam




from UDAKU SPECIAL BLOG https://ift.tt/3m3EQkc
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI