Rais afanya mabadiliko madogo baraza la mawaziri





Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amemuapisha Makamu wa Rais wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango na kisha kufanya mabadiliko madogo katika baraza la mawaziri.


Mabadiliko hayo ametangaza mara baada ya uapisho wa Makamu wa Rais na kusema kuwa amefanya uteuzi wa wabunge watatu ambao ni aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi Dkt. Bashiru Ally, Balozi Liberata Mulamula pamoja na Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk.



Rais amemteua Mhe. Ummy Mwalimu kuwa Waziri wa Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe. Mohammed Mchengelwa Waziri wa Ofisi ya Utumishi na Utawala Bora, aliyekuwa Waziri wa TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo kuwa Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Mhe. Mwigulu Nchemba kuwa Waziri wa Fedha na Mipango, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Palamagamba Kabudi kuwa Waziri wa Katiba na Sheria.



Pia Mhe. Samia Suluhu Hassan amemteua Balozi Hussein Katanga ambaye ni Balozi wa Tanzania nchini Japan kuwa Katibu Mkuu Kiongozi akichukua nafasi ya Balozi Bashiru Ally ambaye ameteuliwa kuwa Mbunge.



Aidha, Mawaziri wote walioteuliwa leo wataapishwa kesho na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Ikulu ya Chamwino Dodoma.


from UDAKU SPECIAL BLOG https://ift.tt/3m8eVry
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI