Shamimu Mwasha na Mumewe Wahukumiwa Kifungo Cha Maisha Jela..Kisa Madawa ya Kulevya





MAHAKAMA Kuu kitengo cha Uhujumu Uchumi na Makosa ya Rushwa, maarufu kama Mahakama ya Mafisadi, imemuhukumu blogger Shamimu Mwasha (41), na mume wake Abdul Nsembo, maarufu kama Abdulkandida (45) kutumikia kifungo cha maisha gerezani baada ya kupatikana na hatia ya kukutwa na dawa za kulevya aina ya Heroine.

Hukumu hiyo imetolewa leo Machi 31, 2021 na Jaji Elieza Luvanda baada yaa kuridhika na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na mashahidi sita wa upande wa mashtaka.

Shamimu anayemiliki Blog ya 8020 na mumewe Nsembo, walikuwa wanakabiliwa na

mashtaka mawili ya kusafirisha dawa za kulevya aina ya heroini gramu 232.70, kosa wanalodaiwa kulitenda Mei mosi 2019 huko Mbezi Beach jijini Dar es. Salaam.



Shamim Mwasha wakiwa na Mumewe, walipofikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza.



from UDAKU SPECIAL BLOG https://ift.tt/2PEiSbn
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI