Watano Wahukumiwa Kunyongwa Njombe





WASHTAKIWA watano waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya mauaji namba 84 ya mwaka 2014 ya Alice Mtokoma (56), mkazi wa kijiji cha Usalule kilichopo mkoani Njombe wamehukumiwa adhabu ya kunyongwa hadi kufa.

 

Wakisomewa shtaka hilo leo Machi 31, 2021 na mawakili wa serikali Andrew Mandwa na Matiko Nyangelo katika kikao cha mahakama kuu kilichofanyika mkoani Njombe mbele ya Jaji Firmin Matogolo, walisema watuhumiwa hao Mei 13,  2012 walimuua  kwa kumpiga Alice Mtokoma kwa kitu chenye ncha kali, kosa ambalo ni kinyume na kifungu cha sheria na 196 na 197, kanuni ya adhabu, sura ya 16, marejeo ya 2019.

 

Wakili Nyangelo alieleza kuwa siku ya tukio hilo, watuhumiwa walimfuata nyumbani kwake marehemu na kumueleza kuna sehemu wanatakiwa kwenda naye ndipo walipotekeleza mauaji hayo.

 

Hukumu hiyo ya kunyongwa hadi kufa kwa washtakiwa hao ilitolewa na Jaji Matogolo katika kikao cha Mahakama Kuu kilichofanyika mkoani Njombe.

 

Alisema washtakiwa waliohukumiwa adhabu hiyo ya kunyongwa hadi kufa ni James Msumule, Emmanuel Ngailo, Izack Ngailo, Anitha Mbwilo na Upendo Mligo.


from UDAKU SPECIAL BLOG https://ift.tt/31ycftI
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI