Bwalya: Tutafanya Maajabu Kimataifa… Droo Ya CAF Leo




KIUNGO mshambuliaji wa Simba, Larry Bwalya amesema kuwa timu hiyo ina nafasi kubwa ya kufanya maajabu katika Hatua ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambayo inatarajiwa kupangwa leo Ijumaa.

 

Bwalya alijiunga na Simba mwanzoni mwa msimu huu baada ya kiwango chake kufurahishwa na mabosi wa timu hiyo.

 

Akizungumza na Championi Ijumaakuelekea kwa droo hiyo ambapo Simba ndiyo itajua mpinzani wake, Bwalya alisema: “Imekuwa heshima kwangu na timu pia kuona tunafanikiwa kutinga hatua ya robo fainali katika michuano ya kimataifa.



“Kwa sasa tunasubiri ratiba na timu ambayo tutacheza nayo katika hatua ya robo fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

 

“Bado tunayo nafasi ya kutwaa ubingwa wa michuano hiyo kutokana na maandalizi mbalimbali ambayo tunaendelea kufanya, “ alisema Bwalya.

 

Katika droo ya leo Simba inatarajiwa kupangwa na wapinzani kati ya hawa, CR Belouizdad au MC Alger zote za Algeria au Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini

Stori: Leen Essau,Dar es Salaam



from UDAKU SPECIAL BLOG https://ift.tt/334zDzP
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI