Prisons: Tutawapiga Yanga Kwenye Mshono




NAHODHA wa kikosi cha Tanzania Prisons, Benjamin Asukile amewachimba mkwara wapinzani wao katika mchezo ujao wa Kombe la FA, Yanga, kwa kusema kuwa wanapaswa kujiandaa kisaikolojia kwani baada ya kufungwa na Azam FC, kipigo kingine kinawasubiri huko Sumbawanga.

 

Prisons, leo Ijumaa itawakaribisha Yanga katika mchezo wa Hatua ya 16 Bora wa michuano ya Kombe la FA, utakaopigwa kwenye Uwanja wa Nelson Mandela uliopo Sumbawanga mkoani Rukwa.

 

Yanga itaingia katika mchezo huo ikiwa na kumbukumbu mbaya ya kipigo cha bao 1-0 walichokipata kutoka kwa Azam FC, Jumapili iliyopita katika Ligi Kuu Bara (VPL).



Kumbukumbu ya mwisho inaonyesha kwenye michezo miwili ambayo timu hizo zimekutana msimu huu kwenye VPL, zilitoa sare pacha ya bao 1-1 mara mbili, Septemba 6 na Desemba 31, mwaka huu.

 

Akizungumza na Championi Ijumaa,Asukile alisema: “Tunaendelea na maandalizi ya mchezo wetu ujao dhidi ya Yanga, tuko tayari na tunawasubiri kwa hamu kwa kuwa siku zote tunapokutana na Yanga au Simba, tumekuwa na mchezo bora na huwa tunawapa changamoto ya kweli.“

 

Tunajua Yanga wanaingia katika mchezo huu wakiwa na maumivu ya kupoteza mchezo wao uliopita wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Azam, lakini hilo sisi halituhusu nasi tumejiandaa kupiga palepale walipopiga Azam, hivyo mashabiki wa Yanga wanapaswa kujiandaa kisaikolojia kwa maumivu.”

 


from UDAKU SPECIAL BLOG https://ift.tt/3vCd0zf
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI