Rais wa Marekani aionya China kuwa hatavumilia chokochoko



Rais wa Marekani Joe Biden amelihutubia bunge la nchi hiyo kwa mara ya kwanza akiwa rais na kutumia sehemu ya hotuba yake kuwaonya washindani namba moja wa kibiashara wa Marekani nchi ya Uchina.

Biden amesema kuwa Marekani haitakaa kimya wakati makampuni ya kichina yakitia usalama wa makampuni ya kimarekakani na hata ajira za raia wake.

Rais huyo amelieleza taifa lake kupitia hotuba hiyo ya bungeni kuwa katika mazungumzo yake na rais Xi Jinping wa Uchina, ameweka wazi msimamo wake kuwa japo Marekani haitafuti mgogoro na Uchina, lakini pia atalinda maslahi yake ya kibiashara kwa nguvu zake zote.

"Marekani itasimama kidete dhidi ya tabia zisizo za mizania katika biashara kutoka Uchina. Mambo ambayo yanawaminya wafanyakazi wa Marekani na viwanda vyao. Mambo hayo ni kama kutoa ruzuku kwa viwanda vinavyoeindeshwa na serikali, wizi wa teknolijia ya kimarekani paoja na hatimiliki ."

Mahusiano baina ya Marekani na Uchina yapo katika kilele cha migogoro kwa sasa.

Mwezi Machi, kabla ya mkutano wa kwanza wa ngazi ya juu baina ya Uchina na Marekani, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken aliielezea China kama, "ndiyo nchi pekee inayoweza kuipa changamoto Marekani katika katika anga za kimataifa kwenye nyanja za uchumi, diplomasia na teknolojia."

Katika hotuba yake, Biden aliitaja China na rais wake takriban mara nnne.

Japo wachambuzi wanaeleza kuwa si lengo la Biden kuendeleza mgogoro na Uchina, lakini rais huyo anatuma ujumbe kuwa hatalegeza kamba katika kukabiliana na nchi hiyo.

Rais Biden ameitoa hotuba yake Jumatano usiku kwa saa za Marekani (sawa na Alhamisi alfajiri kwa Afrika Mashariki) ikiwa ni siku 100 kamili toka alipoingia madarakani.

Biden ametangaza mpango mkubwa wa uwekezaji katika huduma za kijamii da dola trilioni 4 - ambao ni mpango mkubwa zaidi wa huduma za kijamii kwa Marekani toka miaka ya 1960, kwa mujibu wa wachambuzi.

Rais huyo ameuita mpango huo ni "wa mara moja kwa kizazi."

Hata hivyo, mpango huo kwanza utalazimika kupitishwa kwenye Bunge la Congress ambako inategemewa utakumbwa na upinzania kutoka kwa wawakilishi wa Republican.

Wawakilishi wa Republican hawaungi mkono kuongezwa kwa matumizi ya serikali na ongezeko la kodi kwa matajri.

Japo chama cha Biden, Democrat kina wingi wa wajumbe katika mabunge yote mawili ya Marekani lakini wao pia bado kuna misigano ya kwa namna gani na kiwango kipi mpango huo utekelezwe.

 


from UDAKU SPECIAL BLOG https://ift.tt/3aMGFOb
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI