Sheria ya uhujumu uchumi kufumuliwa





Hatua ya Wizara ya Katiba na Sheria kupitia Tume ya Kurekebisha Sheria kufanyia tathmini sheria sita, ikiwamo ya uhujumu uchumi, imepokelewa kwa furaha na wadau wa sheria ikielezwa kuwa ni kilio cha muda mrefu cha kuondoa sheria kandamizi za muda mrefu.
Hatua hiyo imetangazwa na Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi jana, wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2021/2022, akisema lengo ni kufahamu kama sheria hizo zinaweza kutumika katika kupunguza msongamano magerezani.

Mbali na uhujumu uchumi, Profesa Kabudi alizitaja sheria nyingine zinazofanyiwa tathmini kuwa ni pamoja na Sheria ya Magereza, Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai na Sheria ya Huduma za Jamii, Sheria ya Bodi ya Msamaha na Sheria ya Kikomo cha Adhabu.

“Madhumuni ya tathmini hii ni kubainisha kama sheria zilizopo zinaweza kutumika kupunguza msongamano magerezani na hivyo kupunguza gharama za kuendesha magereza,” alisema.

Profesa Kabudi alisema kwa upande wa uboreshaji wa sekta ya utalii, sheria zinazofanyiwa tathmini ni pamoja na Sheria ya Utalii na Sheria ya Wanyamapori.

Nyingine ni Sheria ya Mbuga za Wanyama, Sheria ya Makumbusho ya Taifa, Sheria ya Hifadhi ya Eneo la Mamlaka ya Ngorongoro na Sheria ya Malikale.


from UDAKU SPECIAL BLOG https://ift.tt/2S7tHnu
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI