Shomari Kapombe aongeza mkataba Simba




Beki wa pembeni wa Simba, Shomari Kapombe amesaini dili jipya baada ya kukubaliana na uongozi kuongeza mkataba.

Beki huyo mzawa chaguo namba moja la Kocha Mkuu, Didier Gomes mkataba wake ulikuwa unafika ukingoni mwishoni mwa msimu wa 2020/21.

Alikuwa anatajwa kuingia rada za FAR Rabat ya Morocco pamoja na timu nyingine nchini Afrika Kusini ambazo zilikuwa zinahitaji saini yake.

Baada ya makubaliano mazuri na mabosi wake wa sasa nyota huyo amesaini dili jipya na inaelezwa ni kandarasi ya miaka miwili.


from UDAKU SPECIAL BLOG https://ift.tt/3nx1fHs
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI