Tanzania, Marekani Mambo Safi





SERIKALI ya Tanzania imewahakikishia Wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Marekani mazingira mazuri na kuwasihi kuendelea kuwekeza hapa nchini.

 

Ahadi hiyo imetolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula alipokutana kwa mazungumzo na Balozi wa Marekani nchini Mhe. Donald Wright katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.

 

Balozi Mulamula amesema makampuni mbalimbali kutoka Marekani yameonesha nia ya kuwekeza katika sekta za nishati, miundombinu, afya na kilimo hususani katika zao la korosho.

 

“Katika kikao changu na Balozi tumejadili na kusisitiza umuhimu wa Kampuni za Marekani kuwekeza nchini Tanzania……… na Balozi amenihakikishia baadhi ya kampuni hizo zipo tayari kuwekeza hapa nchini,” amesema Balozi Mulamula

 

Aidha, Waziri Mulamula amewataka wafanyabiashara na wawekezaji wa Kitanzania kujipanga kutumia fursa ya kuuza Marekani bidhaa mbalimbali zinazozalishwa hapa nchini.

 

Kwa Upande wake Balozi wa Marekani, Wright amesema uhusiano wa Marekani na Tanzania ni wa miaka mingi na kuahidi kuuendeleza na kuimarisha uhusiano huo.

 


from UDAKU SPECIAL BLOG https://ift.tt/3nHP6zD
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story