Chombo cha Dola Hakipaswi Kumuadhibu Mtuhumiwa




Wakili maarufu nchin Jebra Kambole amesema vyombo vyenye mamlaka nchini hususan vyombo vya dola havina mamlaka yakumfanyia mtu kama wanavyotaka pindi wanapomtia hatiani kwani kuna sheria ambazo zinaeleza taratibu zinaposwa kufuatwa.
Wakili Kambole ameeleza hayo katika mahojiano na Kipindi cha Supa Breakfast ambapo amesema kitendo kilichofanywa na askari wa Uhamiaji kwa mtuhumiwa kupitia video zilizosambaa mtandaoni kuwa hakikuzingatia utu na wala haki kwa mujibu wa sheria.

“Watu wana viheshimu vyombo vyenye mamlaka na wao kwakuwa wanaheshimiwa hawapaswi kumfanyia mtu ndivyo sivyo, kuna vitu vimetendeka katika tukio hilo mimi naona havipo sawa mtuhumiwa angeweza kusema naomba mnichukulie hatua au apelekwe mahakamani,” amesema Wakili Kamabole.

“Hakuna chombo cha dola kinachoweza kuamua kumtesa mtu wanavyotaka wao, kama kuna mtu kafanya kosa la jinai utaratibu upo kwenye sheria zetu, ukisema kila mtu ajichukulie sheria mkononi hii nchi haiwezi kutawalika,” ameongeza Wakili Kamabole.

Pia Wakili Kambole akielezea haki ambazo mtuhumiwa anazokuwa nazo pindi anapokamatwa na vyombo vya dola amesema mtuhumiwa ana haki ya kutokutweza utu wake.

“Unapokamatwa na vyombo vyenye mamlaka una haki ya kuwasiliana na ndugu yako, mawakili juu ya kukamatwa kwako, una haki ya kutibiwa na kujieleza unapokuwa kwenye vyombo vya dola lakini una haki ya kutopigwa wala kutweza utu wako,” amsema Wakili Kamabole.




from UDAKU SPECIAL BLOG https://ift.tt/3p5FLlG
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI