Mondi Kibo, Konde Boy Mawenzi




Yes Mondi yupo juu zaidi, lakini chini yake kuna Konde Boy. Baada ya hapo kuna gepu kubwa sana mpaka kuwakuta wengine. Bahati mbaya zaidi hata wasanii wameamua kuwa mashabiki. Yaani kuna Team Mondi na Team Konde ya wasanii wenzao.
ADVERTISEMENT
Jamaa wapo juu pale. Yes Mondi yupo juu zaidi, lakini chini yake kuna Konde Boy. Baada ya hapo kuna gepu kubwa sana mpaka kuwakuta wengine. Bahati mbaya zaidi hata wasanii wameamua kuwa mashabiki. Yaani kuna Team Mondi na Team Konde ya wasanii wenzao.

Mlima Kilimanjaro una vilele viwili, Mawenzi na Kibo. Yes! Ni mfano kwa wasanii hawa waliopo vileleni wakiwatazama wenzao kwa chini mitaa ya Marangu. Ukifuatilia mitikasi zao tu kupitia mitandaoni kama Insta. Utaona masela hawa namna wanavyoonyesha kwa vitendo matumizi ya noti wanazoingiza.

Noti, faranga, mkwanja, mapene, mawe, shilingi, paundi, dola unaweza kuita utakavyo. Ndiyo kipimo rahisi zaidi cha mafanikio kwa wasanii na sanaa. Heshima ni moja, utajiri ni jambo lingine tofauti kabisa. Lakini vyote vinahusiana na ukubwa wa mafanikio katika sanaa. Hawa masela wanatumia pesa.

Kuna Darassa nyuma yao. Ambaye naye amekuwa akipambania umwamba huu kwa matumizi ya pesa kwenye muziki. Wakati kulikuwa na ‘kashfa’ ya kutumia pesa kuhonga watangazaji na madj. Madogo wao wana ‘kashfa’ kutumia mkwanja mrefu kutengeneza muziki na video kali.

Kuna wana kitambo hicho wameusotea sana huu muziki. Sasa kuna vijana wanasotea sana mafanikio ya Mondi na Konde Boy. Yaani nao wapo kwenye ‘gemu’ kama wao, lakini minara ya bata na mapato iko tofauti. Zamani kulikuwa na ‘stresi’ za ‘eataimu’, sasa ni ‘stresi’ bata la madogo ‘wanaomeki mane’ kupitia ‘gemu’.

Inawezekana zamani muziki haukulipa sana kwa kiwango hiki cha sasa. Lakini tofauti ya kipato kwa wasanii haikuwa kubwa kama sasa hivi. Kuna uwiano mbovu kwa wenye nazo na kwa wale wenye kiasi. Yaani kutoka Mondi mpaka Konde kuna kilometa nyingi.

ADVERTISEMENT

Sasa huyo ni Konde Boy ambaye Diamond akiwa ‘Sauzi’ yeye yupo Naija. Vipi wengineo ambao Mondi akiwa Hotel Verde Zenji, wao wapo Tanganyika Packers Kawe wakipuliza mimoshi yao? Wale ambao hata instagram wana wafuasi wachache kama ndevu za AY?

Wakati pengo la kipato kwa Mondi na Konde kuna kilometa kadhaa. Basi pengo la Mondi na Konde na wasanii wengine kuna maili nyingi sana. Zamani pamoja na kwamba Ferouz aliuza sana albamu, lakini hakuwa mbali sana kimaisha na TID.

Dai Konde pcc
Wakati hivi sasa Billnass na Konde Boy kuna mlima mrefu sana kimapato. Kwao hakukuwa na tofauti kubwa sana ya Q Chilla na Ngwea kimaisha. Wao walizidiana pango la nyumba na maeneo waliyopanga na kusukuma balloon mjini.

Leo hii aliyepanga Sinza anafanya muziki uleule anaofanya Mondi mwenye majumba mpaka ‘Sauzi’. Muziki wa sasa, wakati mmoja anawaza kuachana nao ili afanye dili la bodaboda, Konde anamnunulia Kajala ndinga ya milioni 16. Na huyo ni Kajala tu ambaye wengi ndio tunayemjua.

Wakati kuna wanamuziki wanahangaika na mikeka ya kubeti mitaani. Huku wengi wakiwa na hamu ya kuandikwa na kina Carry Mastory insta, Diamond anawaponda wenye jarida maarufu na kubwa duniani la ‘Forbes’, kwa kile alichokiita kama ‘listi’ yao ya wasanii matajiri Afrika ni ya kipuuzi.

Wakati mwingine sitaki kuamini kuwa muziki wetu umekua. Bali kuna wasanii kadhaa wamepata mafanikio makubwa sana kwa sababu ya muziki. Mondi na Konde, ni kama vilele vya Mlima Kilimanjaro, yaani Kibo na Mawenzi. Wanaonekana wao tu pale juu.


from UDAKU SPECIAL BLOG https://ift.tt/2TlWfKz
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI