Rais Mwinyi Atoa Msimamo Chanjo ya Corona Zanzibar



Rais Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,  Dkt. Hussein Mwinyi, amesema chanjo ya ugonjwa wa Covid-19 unaosababishwa na virusi vya corona ni hiyari na hakuna mtu yeyote atakayelazimishwa na si lazima kama baadhi ya wananchi wanavyodai kiasi ya kuzusha taharuki.

Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo Mei 29, 2021 wakati wa ziara ya kuwashukuru viongozi wa CCM wa ngazi mbalimbali katika ukumbi wa Mahonda Mkoa wa Kaskazini Unguja, amesema wananchi wasikubali kufikishwa sehemu na kuambiwa wakichanjwa wanakufa.

''Ndugu wananchi napenda kuweka wazi na bayana  suala hili la chanjo ya kujikinga na ugonjwa wa corona ni hiyari na hakuna atakayelazimishwa ingawa kwa upande wa mahujaji Serikali ya Sauda Arabia wametutaka mahujaji watakaofanya ibada hiyo lazima wapewe chanjo,'' amesema Dkt. Mwinyi.

“Nimesema tutaleta chanjo anayetaka akachanjwe asiyetaka aache, tuwaambie watu walielewe jambo hili Serikali hailazimishi mtu na mimi binafsi nisingetaka mtu anilazimishe iwe hiyari yangu nataka nitachanjwa sitaki basi, sina budi lazima nichanjwe vinginevyo siendi hija, hiyo ndio habari ya chanjo tusiwe na maneno mengi kupitiliza,”amesisitiza Rais Dkt. Mwinyi.



from UDAKU SPECIAL BLOG https://ift.tt/3uyYK9d
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI