Simba haikamatiki VPL, yaichapa Namungo 3-1

 


Mabingwa wa ligi kuu Tanzania bara Simba SC imefanikiwa kuondoka na alama tatu dhidi ya Namungo FC baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 na kuendelea kujikita kileleni mwa msimamo wa VPL, wakiongoza Ligi kwa tofauti ya alama tatu.

 

Wenyeji Namungo ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Styve Nzigamasabo dakika ya 22, lakini baadae kipindi cha pili Simba walirudi na kufunga mabao matatu kupitia kwa Chris Mugalu dakika ya 79, John Bocco alifunga bao la pili dakika ya 84 ambalo hili ni bao lake la 11 kwenye ligi kuu lakini ni bao lake la 5 kwenye michezo mitatu ya mwisho kwenye mashindano yote na Bernard Morrison akafunga bao la tatu dakika ya 88.


Kwa ushindi huu Simba wanafikisha alama 64 na wanaendela kusalia kileleni mwa msimamo huku wakiwa wamecheza michezo 26 ikiwa ni michezo mitatu pungufu dhidi ya watani zao Yanga wanaoshika nafasi ya pili ambao wamecheza michezo 29 wakiwa na alama 61.


Namungo wanasalia nafasi ya 8 na alama zao 40 na mchezo wa jioni ya leo ulikuwa ni mchezo wao wa 29 wa ligi kuu.



from UDAKU SPECIAL BLOG https://ift.tt/3c3tQ2G
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI