Wadau wa buruduani Twitter waanzisha kampeni ya kutompigia kura Diamond tuzo za BET kisa kujihusisha na siasa




Kutoakana na taarifa ya kuwa msanii wa Bongo Fleva Diamond Platnumz ameingia katika tuzo za BET katika kipengele cha BEST INTERNATIONAL ACT ambapo anashindana na wasanii wengine kutoka nchini Nigeria kama Burna boy na Wizkid baadhi ya wadau wa burudani kupitia mtandano waTwittwer Tanzania wameanzisha kampeni ya kutompigia kura msanii Diamond kwenye tuzo za BET wakidai kwamba anajihusisha na Siasa za upande mmoja mfano kwenda kupigia kampeni Chama fulani Cha Siasa.

Zifuatazo ni baadhi ya post za wadau hao wakimlaumu Diamond kujihusisha na Siasa wakidai eti aliipigia kampeni Chama fulani hivyo wao kwa sababu wanatoka katika vyama vingine hivyo hawatajihusisha na upigaji kura kwa kumpigia Diamond labda apigiwe kura na Chama hicho licha ya kuwa ni Mtazania mwezao bali watampigia msanii kutoka Nigeria Burna boy.

Ikumbukwe kuwa baadhi ya wasanii wenzake wameanza kumkingia kifua akiwemo Wakazi Irene Paul, Dora na wengine lakini pia Mange Kimambi naye amekuwa msatari wa mbele kumpigania Diamond akisema kuwa anastahili kuchukua tuzo hiyo.



from UDAKU SPECIAL BLOG https://ift.tt/3vDq9IE
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI