Wakazi Achafukwa Waopiga Kampeni Diamond BET Award


ANAANDIKA Wakazi

Nimesikitishwa na comment za watu za kusema hawataki kum-support Diamond BET kwa sababu akishinda ataitumia kama fimbo kuwa mahasimu wake na wengine wanasema hawawezi kum-support msanii ambae alikuwa CCM.

Diamond mimi sio hata rafiki yangu na huwa nina m-criticize mara nyingi tu kama ninavyofanya kwa wengine, lakini penye pongezi apewe, na hii ya BET ina manufaa kwa TZ nzima.

Akiwa nominated na akashinda, basi awareness ya Tanzania katika ulimwengu wa muziki inaongezeka, na ikiongezeka basi nafasi ya msanii unayempenda kupata fursa inaongezeka pia. So hata kama ningekuwa nina mchukia jamaa (which I don’t), naelewa umuhimu wa nafasi aliyopo kwetu Wasanii na kwa Taifa pia.

Tujifunze kujenga UMOJA kupitia TOFAUTI zetu. Badala ya kudumisha CHUKI, basi tutafute suluhu ambazo zina manufaa kwa wengi kama sio wote.

Ni kama hili swala la Ushindani na Ushabiki tumelielewa vibaya hapa Tanzania. Niliwahi ku-rap “SIMBA na YANGA ni wapinzani wa Jadi, ila ukiweka Simba na Yanga unapata TAIFA STARS”. Meaning hapa ndani sawa tushindane, ila huko nje tuungane kwa maslahi zaidi.

Ni kweli akishinda atapata bichwa, hata ungekuwa wewe hilo halipingiki, ILA bado nasi tunanufaika.

Na ukisema kisa ali-support CCM, unakuwa huna tofauti na ambao wanamnyima fursa @wakazi Jhikoman, Vitali Maembe, @officialbabalevo kisa nao walikuwa Upinzani. Basi ningewaona bora zaidi kama mtatu-support sisi tuinuke, na sio kutumia nguvu kumshusha mwingine. Just saying….

“Two wrongs don’t make it right” hata kama yeye kaongea mbovu. Na it’s okay kama hum-support ILA kufanya kampeni kabisa waziwazi, we better than that. Tasnia yetu ina matatizo mengi, ila nadhani tiba ya kwanza inabidi iwe UPENDO.

The Leader.



from UDAKU SPECIAL BLOG https://ift.tt/3fYkuGh
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI