Waziri Mkuu Uingereza afunga ndoa




Waziri Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson amefunga ndoa na Carrie Symonds katika sherehe ndogo iliyofanywa  kwa siri huko Westminster Cathedral.


Boris anakuwa waziri mkuu wa kwanza kufunga ndoa akiwa anaitumikia ofisi ikiwa imepita takribani miaka 200 tangu kutokea kwa tukio la aina hiyo.



Wawili hao waliofunga ndoa jana Jumamosi Mei 29, 2021 huku Waziri Nadhim Zahawi akisema  hakuhudhuria sherehe hiyo lakini amewatakia kheri katika ndoa yao.



"Ninadhani ni jambo la kufurahisha kwa wote wawili kuweka nadhiri zao za ndoa, ninawatakia kila la kheri," amesema Zahawi.



Ingawa Boris alishawahi kufunga ndoa mara mbili,  Kanisa Katoliki linaruhusu watalaka kufunga ndoa nyingine iwapo viapo vya ndoa za zamani vililiwa nje ya kanisa hilo.




from UDAKU SPECIAL BLOG https://ift.tt/3wKKPhQ
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI