RUWASA yaombwa Kuondoa Tenki Kwenye Mkondo wa njia ya Mizimu




Na Timothy Itembe Mara.
RUWASA wanaombwa kuondoa Tenki la maji kwenye mkondo wa njia ya (SABURE)ambaye ni mkuu wa koo ya Wanchari.

Mwenyekti wa Jumuiya ya watumia Maji Korotambe kata ya Mwema wilayani Tarime,Alphons Nyaiho alisema kuwa Ruwasa walijenga Tenki la maji kwenye mkondo wa njia ya Sabure ambaye ni mkuu (MZIMU)wa koo ya Wanchari kabIla la Wakurya bila kuwashirikisha wazee wa milahali ambayo imechangia mradi huo kutotoa maji.

Nyaiho aliongeza kusema kuwa kufuatia hali hiyo mradi wa Korotambe umekumbwa na changamoto kubwa ya kukoswa maji licha ya kuwa mradi umekamilika na wananchi hawafaidi matunda ya mradi huo kwa mda wa zaidi ya mwaka."Mimi niseme kuwa wananchi wa Korotambe wanataabika kwa kutofaidi mradi wao wa maji ambao ulianza mwaka 2012 na kukamilika 2020 kutokana na Ruwasa kujenga Tenki la maji kwenye mkondo wa njia ya Sabure ambaye ni mkuu wa koo ya Wanchari bila kuwashirikisha wazee wa mila hali ambayo imechangia mradi kutokuwa namaji licha ya kuwa umekamilika"alisema Mwenyekiti huyo.

Baada ya hali hiyo kuwepo Kamati ya watumia maji wakishirikiana na Ruwasa waliomba kuonana na wazee wa mila ambapo wazee hao waliomba vifaa kadhaa wakadha vya kimila ikiwemo Mbuzi wa kafara na kufanya matambiko lakini hapo pote mradi hautoi maji na badala yake mradi unaingiza hasara pale ambapo shilingi zaidi ya Alfu themanini zinatumika kwa kupambu maji kwenda kwenye Tanki na kesho yake unakuta maji yamekwisha kwenye Tenki bila kutumiwa na mtu.

Nyaiho alibainisha kuwa wanatumia zaidi ya shilingi 80,000 kupambu maji kwenda kwenye Tanki lakini kesho yake wanajikuta maji yameisha bila kutumiwa na mtu na katika kitendo hicho Jumuiya inaambulia mavuno ya maji ya shilingi 5000 tu ambayo wanauza jambo ambalo ni hasara wanaomba msaada zaidi wa kiutaalamu.

Kwa upande wake Patirisia Joseph kutoka Nyamwaga alitumia nafasi hiyo kuwatupia lawama viongozi wa vijiji na kata kwa maana ya watendaji na wenyeviti kuwa hawatoi ushirikiano kwa jumuiya ya watumia maji jambo ambalo linasababisha mradi kukwama na kushindwa kujiendesha.

Mwana mama huyo aliwataka watu wa Ruwasa kuendelea kutoa elimu ndani ya viongozi na jamii iliyopo ili kuendelea kutoa ushirikiano kwa lengo la kufanikisha malengo ya mradi kwa manufaa ya Taifa na jamii kwa ujumla.

Naye Katibu Tawala wilaya Tarime,John Mrwa kwaniaba ya mkuu wa wilaya ambaye alialikwa kuwa mgeni rasimi katika kikao cha wadau wa Maji kilichoketi katika ukumbi wa Chuo cha walimu TTC Tarime alisema kuwa Serikali inapotekeleza miradi kwa jamii lengwa inamaana miradi hiyo iwanufaishe wanajamii siovinginevyo.

Marwa aliongeza kusema Jamii inatakiwa kulinda na kutunza miundombinu ya mradi iliyotekelezwa na inayoendelea kutekelezwa kwa manufaa yao na vizazi vijavyo vinginevyo kama kuna anaye husika kuhujumu mradi kuna haja ya kumtambua ili kuchukuliwa hatua za kisheria.

Kaimu Meneja Ruwasa,Laurenti Biseko alisema katika kuhakikisha vyombo vya watumia maji vinatoa huduma stahiki kwa mjibu wa sheria ya maji na usafi wa mazingira namba 5(2019)Ruwasa Tarime hufanya ufuatiliaji wa vyombo na shuguli zinazotekelezwa.


from Udaku Special https://ift.tt/3jGVI1d
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI