Wema Sepetu Adaiwa Kenya Kisa Dawa za Kupunguza Unene



Muigizaji wa filamu za Bongo nchini Tanzania Wema Sepetu amejipata pabaya baada ya kifichuliwa kwa kitendo chake cha kukiuka mkataba.

Mwanadada huyo maarufu nchini Tanzania aliingia kwenye mkataba na kampuni moja ya madaktari nchini Kenya kwa jina “Viva Serenity”.

Chini ya mkataba huo, kampuni hiyo ingegharamikia upasuaji wa kumsaidia kupunguza uzani wa mwili naye aifanyie matangazo ya kibiashara kama balozi wake.

Kampuni ilitimiza jukumu lake maanake ghafla Wema alionekana kapungua kimwili lakini hakusema ukweli kuhusu namna aliyotumia kuafikia mwili wake mdogo.


Badala ya kutangaza Viva Serenity na upasuaji wao, Wema alianza kutangaza vidonge vya kumeza akisema ndivyo vilimsaidia kupungua na akawa anaviuza.

Sasa kampuni hiyo ya madaktari ya Kenya inataka muigizaji huyo ambaye aliwahi kuwa mpenzi wa Diamond Platnumz arejeshe pesa ambazo zilitumika kwake au aitangaze walivyokubaliana.

Kwa sasa kampuni hiyo imejiundia video kutokana na safari ya Wema Sepetu ya kupunguza uzani wa mwili na kiweka kwenye mtandao wa YouTube kwa nia ya kujiongezea biashara.


Wametumia picha na video mbali mbali zilizonakiliwa wakati wa kuingia kwenye mkataba na Wema Sepetu na kuonyesha muonekano wake wa awali na wa sasa.

Wema hajasema lolote kuhusu jambo hili lakini Mange Kimambi ambaye pia ni maarufu Tanzania amemshauri atekeleze sehemu yake ya mkataba au arejeshe fedha zilizotumika.

Amemtia moyo akisema upasuaji huo wa kupunguza uzani wa mwili almaarufu “gastric bypass” sio jambo la kuaibikia Kwani nyota wengi Marekani wametumia njia hiyo kupungua na huwa wanasema hadharani.

Mange amefichua kwamba Wema amewahi kumtapeli kwa njia sawia pale ambapo alimtumia wigi kutoka Marekani ili amtangazie biashara yake ya kuuza nywele lakini hakufanya vile.


Kulingana na Mange, Wema alipokea ile wigi, akapigwa picha nayo akabandika mitandaoni, lakini hakutaja biashara yake walivyokubaliana.


from Udaku Special https://ift.tt/2UUaKWU
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI