Yanga: Ubingwa ni Wetu




OFISA Habari wa Yanga, Hassani Bumbuli, amefunguka kuwa, anaona matumani ya kuchukua ubingwa yapo karibu kwa upande wao kutokana na kikosi chao kuzidi kuimarika kila siku.

 

Yanga ipo katika nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu Bara, huku ikiwa na pointi 67 ikiongozwa na kinara wa Simba wenye pointi 73.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Bumbuli alisema kuwa kila kitu kipo katika utaratibu wake katika suala la maandalizi, kwa hiyo wamejipanga kuchukua ubingwa wa FA.

 

“Maandalizi yanaendelea vizuri kama kawaida, niseme tu kwamba tumejipanga kuchukua ubingwa katika pande zote.“

 

Kikosi chetu kinazidi kuimarika kila siku na sitaki kuongea sana, lakini mtajionea wenyewe kinachoenda kutokea, lazima tuchukue ubingwa,” alisema Bumbuli.Julai 25, mwaka huu, Yanga na Simba zinatarajiwa kupambana katika mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam maarufu FA.




from Udaku Special https://ift.tt/3jsnZIw
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI