Zaidi ya watu 100 wapoteza maisha kutokana na joto kali Canada





Watu kadhaa wamefariki nchini Canada kutokana na joto lisilo la kawaida kupiga ambalo limevunja rekodi ya kiwango cha joto.
Polisi wa British Columbia wamepokea taarifa za vifo vipatavyo 70 tangu Jumatatu, vifo vingi vikijumuisha wazee.

Wanasema kiwango hicho cha joto kupiga katika eneo hilo kilisababisha vifo hivyo.

Jumanne, kiwango cha joto nchini Canada kiliongezeka zaidi ikawa siku ya tatu mfululizo -ilikuwa nyuzi joto 49.5 huko Lytton, British Columbia.

Kabla ya wiki hii , kiwango cha joto cha Canada hakikuwahi kuvuka nyuzi joto 45.

"Waangalie majirani zako, familia yako pamoja na wazee unaowajua ," Polisi wa Canada Mike Kalanj, ambaye yuko Vancouver wilaya ya Burnaby, alisema Jumanne.

"Hali ya hewa inaweza kuwa hatari kwa jamii ya watu ambao hawajiwezi hasa wazee na wale wenye matatizo ya kiafya," aliongeza. Ni muhimu tukawajulia hali kila mara."

Kwa mujibu wa polisi , joto hilo linaaminika kuwa limesababisha vifo vya watu 69 katika mji wa Vancouver wilaya ya Burnaby. Wengi wakiwa wazee na waliokuwa na matatizo ya kiafya.

Katika kijiji cha Lytton, mkazi wa eneo hilo Meghan Fandrich amekiambia chombo cha habari cha Globe & Mail kuwa ilikuwa vigumu hata kutoka nje.

"Hali ilikuwa mbaya sana," alisema, na kuongeza kuwa ilimbidi amuhamishe binti yake mdogo kwenda kuishi eneo jingine la British Columbia ambako joto halikuwa kali sana.

"Tunajaribu kuwa ndani kadiri tuwezavyo.Tumezoea joto lakini si kwa kiwango hiki ambacho kimezidi nyuzi joto 30, ni kingi mno yani kinafika mpaka 47 hivyo utofauti ni mkubwa sana."

Mamlaka ya mazingira Canada imetoa angalizo juu ya jimbo la British Columbia na Alberta, pamoja na maeneo ya Saskatchewan, the Northwest Territories na baadhi ya sehemu ya Yukon.

"Taifa letu ni la pili kwa kuwa na baridi duniani na kuwa na barafu," alisema David Phillips, mtaalamu wa mazingira Canada.

"Tukiongelea suala la joto kuwa kali tunaweza kusema Dubai lakini hali ya joto tunayoiona hapa ni mbaya zaidi ya Dubai."

Joto katika miji ya Marekani ya Portland na Seattle liliwahi kuvunja rekodi mwaka 1940.

Portland ya Oregon ilipiga nyuzi joto 46.1C (115F) na Seattle nyuzi joto 42.2C (108F), kwa mujibu wa mamlaka ya huduma ya hali ya hewa



from Udaku Special https://ift.tt/3hoEG5b
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI