Diamond afurahia kufikisha viewers mil 2 kwa siku mbili, Alikiba afikisha mil 2 ndani ya siku moja

 
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Diamond ameandika kuwa Thank U Our Real Fans For 2Million Views in 2 Days …. Keep Watching #IYO Full Video.

Baada ya muda mfupi Alikiba naye alifanikiwa kufikisha viewers milioni mbili ndani ya siku moja.

Ikumbukwe kuwa nyimbo hizo mbili ziliingia kwenye rekodi mpya baada ya kufikisha viewers mil moja kwenye mtandao wa YouTube kwa kupishana saa moja tu.

Iyo ya Diamond ambayo imeachiwa siku mbili zilizopita ilifikisha viewers milioni moja ndani ya masaa 13 huku Jealous ya Alikiba ikifikisha viewers milioni moja ndani ya msaa 12 na kuwa nyimbo za kwanza Tanzania kufikisha viewers hao ndani ya masaa machache tu.

Baada ya hapo mchuano ulianza ambapo Iyo ilifikisha viewers milioni mbili ndani ya siku mbili huku Jealous ya Alikiba ikifikisha viewers milioni mbili ndani ya siku moja.

Diamond katika ngoma yake ya IYO amewashirikisha wasanii kutoka nchini Afrika Kusini ambao ni Focalist,Mapara A Jazz & Ntosh Gazi huku Alikiba akimshirikisha msanii kutoka nchini Nigeria Mayorkun.


from Udaku Special https://ift.tt/3igwNjS
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI