Jiko la mkaa laua tena Njombe ni baada ya mwingine kulala na jiko kwenye kibanda cha biashara




Na Amiri Kilagalila,Njombe

Edita Mangita (40) mkazi wa mtaa wa Matema kata ya Maguvani mjini Makambako amefariki dunia baada ya kujifungia na jiko la mkaa Katika kibanda chake cha biasahara.

Kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Hamisi Issa amesema tukio hilo limetokea Julai 28,2021 ambapo marehemu Editha aliamua kubaki na kulala katika kibada chake cha biashara Ili kuwahi wateja wake wa asubuhi.

Aidha kamanda Issa amewataka wananchi wa mkoa wa Njombe kuacha kulala na majiko ya mkaa ndani huku akitoa wito kwa wataalamu wa afya kuendelea kutoa elimu kuhusu madhara hayo Ili kuiokoa jamii.

Hivi karibuni mjini Njombe kulitokea  kifo cha watu wawili wapenzi baada ya kulala na jiko la mkaa ili kupunguza baridi katika chumba chao.

Kamanda Issa ametaja tukio lingine la mwanamke mmoja Imelda Mgeni ametelekeza mtoto mwenye umri wa miezi mitatu kwa mume wake naye kwenda kusikojulikana.



from Udaku Special https://ift.tt/3zRZ0mY
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI