Korti yatupilia mbali ombi la utetezi kesi ya Sabaya



 
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha, imetupilia mbali ombi dogo la mawakii wa utetezi katika kesi ya aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya la kutaka ya maelezo awali yaliyoandikwa katika Kituo Kikuu cha Polisi cha Arusha.

Maelezo hayo ni yale yaliyoandikwa na shahidi wa sita wa Jamhuri katika kesi hiyo, Bakari Msangi (38). Mawakili hao waliomba maelezo hayo yatumike kama sehemu ya kielelezo cha ushahidi kwa kuwa utaratibu wa uwasilishwaji ulikosewa.

Mbali na Sabaya, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Sylvester Nyegu (26) na Daniel Mbura wanaokabiliwa na mashtaka matatu ya unyang'anyi wa kutumia silaha.

Akitoa uamuzi huo mdogo, Hakimu Mkazi Mwandamizi Odira Amworo, alitupilia mbali ombi hilo kutokana na sababu mbalimbali baada ya la Mawakili wa Utetezi kutumika kama sehemu ya kielelezo cha ushahidi katika kesi hiyo.

"Baada ya kusoma uamuzi wa pande zote mbili, mahakama ilirejea kwenye baadhi ya kesi katika Mahakama ya Rufani na iliainisha utaratibu wa kufuata moja maelezo ya shahidi yanatakiwa kusomwa, alisema Hakimu Mkazi Odira Amworo wakati akitoa uamuzi huo.


 
“Pili shahidi lazima arejeshwe kwenye maeneo la ushahidi wake ambao unatakiwa kutikiswa na tatu lazima nyaraka itolewe kama ushahidi mahakamani. Katika  hatua ya kwanza haikutekelezwa, hivyo mahakama imekubali kuwa pingamizi limekubaliwa," aliongeza.

Juzi wakati mawakili wa utetezi wakimhoji shahidi huyo wakiongozwa na Wakili Moses Mahuna, waliiomba mahakama watumie kielelezo cha maelezo ya awali ya shahidi huyo kama sehemu ya ushahidi mahakamani.

Baada ya ombi kutolewa, kulitokea mabishano makali ya kisheria kati ya upande wa Jamhuri na wa utetezi.


Mawakili wa Jamhuri wakiongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu Tuamini Kweka, Wakili wa Serikali Mwandamizi Abdalah Chavula na Wakili wa Serikali Baraka Mgaya, walipinga ombi la utetezi kwa madai kuwa hawakufuata utaratibu wa kisheria na wa kimahakama.

Wakili Chavula alidai mahakamani hapo kwamba kuna utaratibu wa kuwasilisha ombi hilo ambao haukufuatwa, hivyo kuiomba mahakama kutupilia mbali ombi hilo.

"Mheshimiwa Hakimu kwa kuwa ndugu zetu wa utetezi hawakufuata kanuni na utaratibu wa kimahakama kuomba nyaraka hii kutumika kama sehemu ya ushahidi, tunaomba mahakama yako tukufu itupilie mbali ombi lao,"alidai Chavula.

Mbali na mawakili wa Jamhuri kuiomba mahakama hiyo kukataa nyaraka ya maelezo hayo kutumika kama sehemu ya ushahidi, pia shahidi naye aliiomba mahakama hiyo kutumia ushahidi alioutoa mahakamani badala ya maelekezo alioandikisha kituo cha polisi Februari 9 na 16, mwaka huu.



from Udaku Special https://ift.tt/2TITjIu
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI