Mnyika awataka wananchi kuchukua hatua kupinga kukamatwa Mbowe



Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeitangaza siku ya tarehe 5 Agosti mwaka huu kama siku ya kupinga kukamatwa na kufunguliwa mashitaka kwa Mwenyekiti wa Chama hicho Freeman Mbowe .

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam leo, Katibu Mkuu wa Chama hicho ,John Mnyika  amedai  kilichofanyika kwa Mwenyekiti huyo ni uendelezaji wa ukandamizaji wa demokrasia nchini.

“Mbowe alikuwa kwenye kazi ya kutetea Katiba Mpya ,Mbowe alikuwa kwenye kazi ya ujenzi wa chama ,Mwenyekiti  Freeman Mbowe anapaswa kuachiwa huru mara moja” –John Mnyika

“Chama kimeacha uhuru kwa wananchi , wanachama  na viongozi wa chama katika ngazi mbalimbali waweze kuandaa matukio ya kupinga mashtaka ya ugaidi dhidi ya Mwenyekiti  Freeman Mbowe na matukio ya kudai Katiba mpya katika siku hiyo “ John Mnyika

Chama hicho pia kimesema baada ya tarehe hiyo kitapanga upya ratiba za makongamano kwa ajili ya Katiba Mpya kwa nchi nzima.


from Udaku Special https://ift.tt/3C2fJWp
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI