Picha chafu zilizomfanya P Mawenge kuachika

 


Rapa Positive Mawenge Kiwalani Kid amefunguka msala aliowahi kukutana nao kwenye mahusiano baada ya mwanamke mmoja kumtumia picha zisizokuwa na maadili wakati huo akiwa na mpenzi wake.

P Mawenge anasema kitendo hicho kilimfanya kuachwa na mpenzi wake huyo waliodumu kwenye mahusiano kwa kipindi cha miaka minne japo alijitahidi kujitetea lakini ikashindikana.

"Kuna mwanamke alinitumia picha WhatsApp sasa mpenzi wangu akaona picha za ajabu ajabu zinaingia iliniletea matatizo sana,  ni mtu ambaye tulikuwa tumezoeana mpaka mnazinguana halafu ile miyayusho inakuja kudondokea kwenye wakati usio rasmi au sahihi"

Aidha msanii huyo ameongeza kusema "Niliachika kwa sababu ya drama unajua ulimwengu wa sasa hivi una sababu nyingi sana za watu kugombana kwenye mahusiano na utandawazi ndio umeleta matatizo tofauti na zamani".



from Udaku Special https://ift.tt/3j9HYd5
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI