Serikali Yavunja Ukimiya Magari Matatu Ya Diamond




MAMLAKA ya Mapato Tanzania – TRA imevunja ukimya kuhusu gharama za magari ya kifahari ya staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ aina ya Cadillac Escalade na Rolls Royce Cullinan, IJUMAA lina stori maalum (exclusive story).


Hatua hiyo imekuja baada ya Diamond au Mondi asiyeishiwa vibweka mjini, kuonekana maeneo ya Kawe na Mbezi-Beach jijini Dar, akiwa anaendesha gari lake ya kifahari aina ya Rolls Royce Callinan Black Badge 2021 bila kuwa na namba ya usajili (plate number), hali iliyozua mjadala mitandaoni kuhusu uhalali wa kutumia gari hilo bila nambari za usajili.




Gari hilo ambalo iliingia nchini mwezi uliopita na kuzua tafrani mitandaoni, hasa ikizingatiwa ni mojawapo ya magari ya kifahari duniani kwani inakadiriwa kuwa na thamani ya zaidi ya shilingi bilioni moja za Kitanzania.

Ujio wa gari hilo pia uliwaibua viongozi wa kisiasa pamoja na wasanii wenzake ambao baadhi yao walimpongeza kwa hatua aliyofikia huku wengine wakimkejeli kuwa gari hilo ni feki, siyo orijino na wala siyo jipya kama anavyosema Mondi, bali amelinunua kwa mtu.“Gari ambalo amenunua Diamond.


 
TRA HAWA HAPA
Kufuatia mkanganyiko wa taarifa hizo, Gazeti la IJUMAA limezungumza na Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Richard Kayombo ambaye anafafanua kwa kina kuhusu magari hayo matatu mapya ya Mondi.




“Unajua sisi sheria haituruhusu kabisa kuzungumzia masuala ya Diamond kulipa kodi na gharama za hayo magari tangu huko yalikotoka hadi hapa (Tanzania) kwa sababu ni mambo binafsi ya mtu, labda yeye mwenyewe ndiye aamue kuwaambia, lakini siyo sisi,” anaanza kusema Kayombo.Akizungumzia kuhusu kutembea na gari bila kuwa na kibao cha namba za usajili, Kayombo anasema; “Lazima atakuwa ana namba ya usajili ila hajaiweka maana gari lolote linapoingia nchini lazima lisajiliwe na kupewa hizo namba.”


GHARAMA ZA NAMBA BINFSI
Moja kati ya mambo ambayo yalishika vichwa vingi vya habari huko mitandaoni ni pamoja na uwepo wa tetesi kuwa, msanii huyo kwa sasa anataka kuweka jina binafsi kwenye magari yake hayo ndiyo maana amechelewa kuweka ‘plate number’ ya kawaida.




“Diamond siyo kama hana plate number, anazo sana, ila anataka kuweka jina lake kwenye magari yake yote na bei zake siyo rahisi kama watu wanavyofikiria, kwa hiyo waache kuongea sana,” anasema mmoja wa watu wa karibu wa Mondi.
Kuhusu hilo, Gazeti la IJUMAA lilimuuliza Kayombo ili kutaka kujua gharama zake ambapo pamoja na mambo mengine, anasema siyo jina tu, kwani hata mmiliki wa gari akitaka kuweka herufi moja garama zake zinafanana.Kayombo anasema gharama za plate number hizo kwa kila gari moja ni shilingi milioni tano ndani ya miaka mitatu na plate number za kawaida gharama zake ni shilingi elfu 20 mpaka pale gari itakapoisha matumizi yake.


TUJIKUMBUSHE
Hadi sasa, Mondi kwenye parking yake kuna magari ya kifahari na ya bei mbaya kama vile Cadillac Escalade (yapo mawili), Rolls Royce, Toyota Land Cruiser V8 (yapo mawili) Toyota Prado pamoja na BMW X6 na amekuwa msanii wa kwanza Afrika Mashariki kumiliki gari aina Rolls Royce.


from Udaku Special https://ift.tt/2UZaO8h
via IFTTT

Comments

Popular posts from this blog

MASHAIRI MATAMU YA MAPENZI

What Happened To Sarafina Skin? From Brown To White Skin – How Did It Happen? Explore The Real Story